Smoke Two Joints

"Smoke Two Joints" ni wimbo ulioandikwa awali na "The Toyes", ambao waliuimba kwa mtindo wa Reggae na kuutoa mwaka wa 1983. Kulingana na "The Toyes", "siku moja tulivu na nzuri iliangukia kwenye kisiwa kidogo cha Oahu huko Hawaii, washiriki wawili wa bendi hio, Mawg na Sky, walikuwa wameketi chini ya mti mkubwa wa banyan kwenye ufukwe wa Kuhio,[1] wakivuta bangi" ndipo ambapo walikuja na wazo la nyimbo hii "Smoke Two Joints."

Nyimbo hii ilitumika kwenye wimbo wa filamu ya kuchekesha ya Marekani ya 1998 iitwayo Homegrown.[2] Toleo la "The Toyes" lilionyeshwa katika mchezo wa video wa 2005 NARC. Wimbo huu mara nyingi unahusishwa kimakosa na Bob Marley kwenye mitandao na tovuti za kijamii. Marley alikuwa ameshafariki miaka miwili wakati wimbo huu ukiandikwa.

  1. "Smoke Two Joints". www.thetoyes.com. 2011. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 6 Februari 2011. Iliwekwa mnamo 15 Machi 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "The SoundtrackInfoProject: Homegrown (1998)".

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy